PROTINI (PROTEIN)
Waswahili husema mwili haujengwi kwa matofali kinyume chake hujengwa kwa kula vyakula bora, na kama tulikuwa hatufahamu basi mjenzi bora wa miili yetu ni protini, hili ndo kundi la chakula lilovaa dhamana ya matengenezo yote ya mwili. Jinsi ulivyo mrimbwende na mtanashati basi ni matokeo mazuri ya protini. Miongoni mwa mafanikio makubwa yanatokea ndani ya mwili wa binadamu basi neno protini huwezi kuacha kulitaja kila hatua. Protini ni sehemu muhimu sana kwa mifumo yote ya maisha ya binadamu kuanzia uzalishaji, mmengenyo wa chakula,upumuaji,utoaji taka mwili,mzunguko wa damu na ukuaji pamoja na muonekano wa mwili kama vile ngozi,kucha na nywele, vyote hivi vinategemea protini kuweza kufanyika. Protini ni miongoni mwa kundi kubwa la chakula ambalo mwili wa binadamu unahitaji kwa kiwango maalum kulingana na umri,kazi na wakati mwingine mazingira ambayo anaishi. Kitaalamu protini ni molecule kubwa zilizoundwa kwa amino asidi. Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha protini Mayai Ni miongo...