PROTINI (PROTEIN)

Waswahili husema mwili haujengwi kwa matofali kinyume chake hujengwa kwa kula vyakula bora, na kama tulikuwa hatufahamu basi mjenzi bora wa miili yetu ni protini, hili ndo kundi la chakula lilovaa dhamana ya matengenezo yote ya mwili. Jinsi ulivyo mrimbwende na mtanashati basi ni matokeo mazuri ya protini.
Miongoni mwa mafanikio makubwa yanatokea ndani ya mwili wa binadamu basi neno protini huwezi kuacha kulitaja kila hatua. Protini ni sehemu muhimu sana kwa mifumo yote ya maisha ya binadamu kuanzia uzalishaji, mmengenyo wa chakula,upumuaji,utoaji taka mwili,mzunguko wa damu na ukuaji pamoja na muonekano wa mwili kama vile ngozi,kucha na nywele, vyote hivi vinategemea protini kuweza kufanyika. 

Protini ni miongoni mwa kundi kubwa la chakula ambalo mwili wa binadamu unahitaji kwa kiwango maalum kulingana na umri,kazi na wakati mwingine mazingira ambayo anaishi.
Kitaalamu protini ni molecule kubwa zilizoundwa kwa amino asidi.

Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha protini
Mayai
Ni miongoni mwa vyakula vyeye kiwango kikubwa cha protini na rahisi kufyonzwa na mwili, na kiwango hiki hupatikana sana kwenye ule ute mweupe tunaouona kwenye yai. Vilevile mayai huupatia mwili vitu vingine adimu na muhimu kama vile vitamini na madini.

Maziwa
Maziwa yana kiwango kikubwa cha protini kutosheleza mahitaji ya mwili, jitahidi unywe walau glasi moja kwa kila siku kwani maziwa pia hutoa kila kitu ambacho mwili unahitaji.

Samaki
wengi wetu hupenda samaki hasa kwa utamu wake ila ni moja ya chakula bora na chenye kiwango kikubwa cha protini.

Maharage
mtaani huko tunayaita mandondo ni chakula kizuri sna chenye protini nyingi tusidharau maharage tuyale kwa moyo wetu wote.
nyama,lozi(almonds),kunde,choroko,mbaazi,dagaa,kweme ni miongoni mwa vyakula vyenye protini kwa wingi.

Kiwango cha protini kinachohitajika mwilini
Kiwango cha chini kabisa kinachohitajika ni wastani gramu 0.8 kwa kilo moja ya uzito wa mtu.
hivyo ukiwa na kilo 10 utahitaji gramu 8 za protini.
lakini inashauriwa kwa watoto, na watu wenye kazi zinazowashughulisha sana,wajawazito na wanaonyonyesha wanatakiwa kupata walau gramu 1.2-2 kwa kilo moja ya uzito wao wa mwili. 
kwa lugha rahisi watu hawa wanahitaji kiwango kikubwa cha protini kila siku hivyo wajitahidi milo yao iwe na vyakula vyenye protini.

Faida za protini mwilini
Kujenga mwili, protini ndiyo inayohusika na ukuaji wa mifupa nauimara wa misuli.

Uboreshaji tishu za mwili, prorini huhusika pakubwa pale unapopata jeraha ama kuumia kwa kiungo ndani ya mwili ili kuweza kurejesha katika hali yake ya awali.

Usafirishaji mwilini, protini huhusika kikamilifu katika kuchukua vitu kutoka eneo moja kwenda lingine mfano haemoglonini zinazosafirisha hewa ya oksijeni kutoka kwenye mapafu kwenda sehemu mbalimbali za mwili.
kukuza nywele, usihangaike sana na mafuta mengi kula vyakula vya protini na utaona afya ya nywele zako ikiimarika vyema.

Ulinzi na kinga ya mwili, antioksidanti zinazopambana na vitu vigeni mwilini huundwa kwa protini hivyo kuusaidia mwili kupambana na maradhi.

Unapojipongeza na kufurahia namna ulivyo, una nywele mzuri,kucha nzuri mwili uliojengeka vizuri tambua pia mchango wa protini.

Comments

  1. Proteins are so important this way, I never know
    Thanks

    ReplyDelete
  2. Ninaomba kufahamu Kiwango cha protini anachotakiwa kutumia mtu mmoja kwasiku

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kiwango cha protini mwili hutegemea umri na shughuli anazofanya mtu. Ila unaweza kuangalia zaidi kwenye jedwali kupitia hizi link hapa chini.

      https://cdn.newsapi.com.au/image/v1/d213b42f66a638aac5fea4ed15ca7c2a

      Delete

Post a Comment

Popular posts from this blog

VYAKULA VYA WANGA (CARBOHYDRATES)

MBOGA /VEGETABLES