Posts

Showing posts from August, 2020

MBOGA /VEGETABLES

Ni matumaini yangu unaendelea vyema na shughuli za kila siku, tukiwa kwenye muendelezo wa faida za vyakula vyetu leo tunaangalia faida zinazopatikana katika mboga za majani. Iwe asubuhi mchana ama jioni basi hakikisha mlo wako unakuwa na mboga za majani. Imezoeleka sana kwamba kula mboga za majani ni ishara ya kuwa na kipato cha chini hali inayopelekea mboga za majani kubakia kuliwa vijijini na watu wasioweza kununua nyama ama samaki jambo ambalo si kweli, mboga za majani ni kwa watu wote wa rika zote na hii ni kutokana na faida tele zinazopatikana kwenye mboga. Nikushauri tu kama hujawahi kufikiria kula mboga za majni basi fanya kama ilkuwa ndoto na mlo ujao ule mboga za majani. Ni zipi mboga za majani? Ni imani yangu tunazifahamu aina nyingi za majani tunazifahamu na ni rahisi sana kupatikana. Si vibaya tukizitaja japo chache; mchicha,sukuma wiki,pilipili boga/hoho,bamia,karoti,giligilani,kabichi,bilingani, nyanya chungu. Tuangalie picha hapo chini bila shaka tuazigundua nyingi...