Posts

Showing posts from April, 2019

VYAKULA VYA WANGA (CARBOHYDRATES)

Image
Vyakula vya Wanga (Carbohydrates) Je, umeshawahi kujiuliza kwanini; (a) Unakua dhaifu na legelege pale unapokua na njaa? (b) Kwanini unakua hodari na mchangamfu pale unapokua umeshiba? Bila shaka wakati wa njaa hua ni dhiki kubwa sana kwako  na haya ndiyo yaliyojiri; Mwili kukosa nguvu,hali inayopelekea kushindwa kufanya kazi,kushiriki michezo. Akili kuchoka haraka na wakati mwingine kushindwa kufanya kazi hali inayopelekea kushindwa kufikiri na kujifunza vizuri. Wengine hupata maumivu ya kichwa. Kinyume cha hayo ni wakati umeshiba unafurahi vizuri hata akili hufanya kazi vizuri hii ni kwasababu mwili umepata nishati kutoka kwenye chakula ulichokula kwa maana nyingine unasema "sasa nina nguvu" . Mwili umendwa na seli ambazo ni mhimili muhimu wa ufanyaji kazi wa mwili.Seli zote za mwili ziwe za misuli,ubongo,ini.. zinahitaji nishati ili ziweze kufanya kazi. Kama seli zitakosa nishati ni wazi kwamba mwili pia hautakua na kazi. Hivyo basi ni muhimu sana...

Mlo kamili(Balanced diet)

 Je tunakula mlo kamili? Jibu lako huenda likawa ndio au hapana na mwingine asijue kabisa kuhusu mlo kamili. Ila maelezo yafuatayo yatatutoa katika kiza na kutuweka kwenye mwangaza juu ya mlo kamili. MLO KAMILI ; ni ule unaozingatia uwepo makundi yote matano ya chakula yaani vyakula vya wanga,protini,matunda,mboga za majani pamoja na vile vya mafuta.                           Na mlo sahihi huenda sambamba na mtindo mzuri wa maisha, kama vile kujiepusha na unywaji wa pombe uvutaji wa sigara matumizi ya dawa za kulevya na mambo mengine ambayo ukiyafanya yanadhuru afya yako.  Na kuzingatia wakati maalum wa kula chakula si kula mara kwa mara inashauriwa hivyo. Kupata mlo sahihi hakuhitaji uwe na pesa nyingi, kwani kuna baadhi wana pesa lakini bado hawafikii mlo sahihi. Ni namna utakavyopangilia ni vipi kwa siku mwili wako utapata faida zinazotokana na makundi yote ya vyakula tuliyotaja hapo juu. Kwa maana tul...

CHAKULA NI TIBA

Utangulizi Habari, natumai umzima wa afya na unaendelea vyema na shughuli za kila siku. Nipende kukukaribisha katika blog hii  ambayo itakukumbusha na,kukujuza juu ya faida zinazopatikana katika vyakula vyetu vya kila siku. Kupitia blog hii utaweza kijifunza mtindo mzuri wa maisha hususa ni katika suala zima la mlo wako wa kila siku. Kwani kula mlo sahihi ni moja ya tiba na kinga dhidi ya maradhi na matatizo mbalimbali ya kiafya ambayo yamekuwa changamoto kwa kiwango kikubwa katika jamii yetu. Ndio sababu iliyopelekea blog hii kuitwa CHAKULA NI TIBA. "Turejee Edeni maana matunda na mboga(chakula) ni dawa." Asema Dr. Jethro. Nikuombe uwe nami katika blog hii na uwajuze wengine ili kuweza kunufaika na yote yatakayojiri ndani ya blog hii .