FRUITS/MATUNDA
Kama kuna jambo ambalo si geni basi matunda ni miongoni mwao, kwani ni chakula ambacho hupatikana sehemu zote ambazo miale ya jua hutua. Matunda hutofautiana kutoka sehemu moja na nyingine kuzingatia hali ya hewa inayoruhusu ustawi wa tunda husika, mfano wenzetu wa Dodoma hufurahia zabibu, Tanga hufurahia embe, peasi na kwingineko ulimwenguni hufurahia matunda yao. Tunda ni nini? Kwa lugha ya mimea tunda ni ovari iliyopea (kwa lugha rahisi iliyokomaa) na sehemu zake ikiwemo ganda na mbegu, ingawa mara nyingi tunaposikia tunda tunafikiri ni yale malaini na matamu. Tunda huweza kuwa limekauka ama kuwa na majimaji. mfano kama vile matango, nazi, machungwa, maharage pamoja na ganda lake, ndizi, njugu/karanga ndani ya ganda lake na mengine mengi tunayoyaona katika maisha ya kila siku. (Tukumbuke kuwa ovari ni sehemu ya kike ya ua). Je, mimea yote hutoa matunda? Si mimea yote huzaa matunda bali kundi moja la mimea ndio lina uwezo wa kutoa matunda, na hili huitwa "mimea inayo...