Posts

VIGINAL TIGHTENING CAPSULE (DAWA YA KUBANA UKE, KUURUDISHA KUWA MDOGO,REJESHA USICHANA)

Image
Habari njema kwa wale wote walioko matatizoni au hatarini kwenye mahusiano yao hususa wanawake kwa hali za kimwili. Khayjam Ayurveda wameleta suluhu ya kuondosha kabisa matatizo yafuatayo; 1. Uke legelege(Tepetepe) 2. Uke unaotoa harufu mbaya baada tendo 3. Uke unaotoa mashuzi mfano wa kujamba 4. Uke Uke wenye maambukizi 5. Uke unaotoka maji meupe 6. Uke mkavu 7. Kukosa kabisa hisia Ukiwa una tatizo miongoni mwa hayo au unamjua mtu ana matatizo hayo basi mwambi3 awasiliane nasi kwa nambari 0778009486 ili aweze kupata tiba sahihi itakayomrejesha usichana na mwenye furaha.

JINSI YA KUZUIA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA WAKATI WA UJAUZITO

Image
Utangulizi Sote ni mashahidi wa kichefuchefu na kutapika hususa wakati wa mimba, kama si mkeo basi huenda akawa dada,shangazi binamu au basi. Naomba niwatoe wasiwasi na taharuki juu ya hili kwani asilimia kubwa ya wajawazito hupitia hiki kipindi kutokana na mabadiliko makubwa yayofanyika mwilini na zaidi yanachangiwa na vichochezi vya homoni. Hali hii husababisha wengi wao kudhoofu na kushindwa kufanya shughuli zao kwa kukosa kula ama kula kisha kutapika chakula chote kwani mwili hukosa nguvu. Nini kifanyike? Wakati huu usikimbilie famasi kutafuta dawa kwani nako pia hawashauri sana mjamzito kutumia dawa za kuzuia kutapika. Badala yake fanya yafuatayo; TANGAWIZI Tangawizi ina uwezo mkubwa wa kuzuia kichefuchefu na kutapika na kuongeza ufanisi wa tumbo kufanya kazi yake ipasavyo. Jinsi ya kutumia 1.Osha wastani wa vidole vitano vya Tangawizi mbichi ikisha visage vizuri. 2.Chemsha kwenye maji ya ujazo wa lita moja kwa muda usiopungua dakika kumi (10), ikisha chuja vizuri na uhifadhi kwen...

FRUITS/MATUNDA

Kama kuna jambo ambalo si geni basi  matunda  ni miongoni mwao, kwani ni chakula ambacho hupatikana sehemu zote ambazo miale ya jua hutua. Matunda hutofautiana kutoka sehemu moja na nyingine kuzingatia hali ya hewa inayoruhusu ustawi wa tunda husika, mfano wenzetu wa Dodoma hufurahia zabibu, Tanga hufurahia embe, peasi na kwingineko ulimwenguni hufurahia matunda yao.  Tunda ni nini? Kwa lugha ya mimea tunda ni ovari iliyopea (kwa lugha rahisi iliyokomaa) na sehemu zake ikiwemo ganda na mbegu, ingawa mara nyingi tunaposikia tunda tunafikiri ni yale malaini na matamu. Tunda huweza kuwa limekauka ama kuwa na majimaji. mfano kama vile matango, nazi, machungwa, maharage pamoja na ganda lake, ndizi, njugu/karanga ndani ya ganda lake na mengine mengi tunayoyaona katika maisha ya kila siku. (Tukumbuke kuwa ovari ni sehemu ya kike ya ua). Je, mimea yote hutoa matunda? Si mimea yote huzaa matunda bali kundi moja la mimea ndio lina uwezo wa kutoa matunda, na hili huitwa "mimea inayo...

MBOGA /VEGETABLES

Ni matumaini yangu unaendelea vyema na shughuli za kila siku, tukiwa kwenye muendelezo wa faida za vyakula vyetu leo tunaangalia faida zinazopatikana katika mboga za majani. Iwe asubuhi mchana ama jioni basi hakikisha mlo wako unakuwa na mboga za majani. Imezoeleka sana kwamba kula mboga za majani ni ishara ya kuwa na kipato cha chini hali inayopelekea mboga za majani kubakia kuliwa vijijini na watu wasioweza kununua nyama ama samaki jambo ambalo si kweli, mboga za majani ni kwa watu wote wa rika zote na hii ni kutokana na faida tele zinazopatikana kwenye mboga. Nikushauri tu kama hujawahi kufikiria kula mboga za majni basi fanya kama ilkuwa ndoto na mlo ujao ule mboga za majani. Ni zipi mboga za majani? Ni imani yangu tunazifahamu aina nyingi za majani tunazifahamu na ni rahisi sana kupatikana. Si vibaya tukizitaja japo chache; mchicha,sukuma wiki,pilipili boga/hoho,bamia,karoti,giligilani,kabichi,bilingani, nyanya chungu. Tuangalie picha hapo chini bila shaka tuazigundua nyingi...

PROTINI (PROTEIN)

Waswahili husema mwili haujengwi kwa matofali kinyume chake hujengwa kwa kula vyakula bora, na kama tulikuwa hatufahamu basi mjenzi bora wa miili yetu ni protini, hili ndo kundi la chakula lilovaa dhamana ya matengenezo yote ya mwili. Jinsi ulivyo mrimbwende na mtanashati basi ni matokeo mazuri ya protini. Miongoni mwa mafanikio makubwa yanatokea ndani ya mwili wa binadamu basi neno protini huwezi kuacha kulitaja kila hatua. Protini ni sehemu muhimu sana kwa mifumo yote ya maisha ya binadamu kuanzia uzalishaji, mmengenyo wa chakula,upumuaji,utoaji taka mwili,mzunguko wa damu na ukuaji pamoja na muonekano wa mwili kama vile ngozi,kucha na nywele, vyote hivi vinategemea protini kuweza kufanyika.  Protini ni miongoni mwa kundi kubwa la chakula ambalo mwili wa binadamu unahitaji kwa kiwango maalum kulingana na umri,kazi na wakati mwingine mazingira ambayo anaishi. Kitaalamu protini ni molecule kubwa zilizoundwa kwa amino asidi. Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha protini Mayai Ni miongo...

VYAKULA VYA WANGA (CARBOHYDRATES)

Image
Vyakula vya Wanga (Carbohydrates) Je, umeshawahi kujiuliza kwanini; (a) Unakua dhaifu na legelege pale unapokua na njaa? (b) Kwanini unakua hodari na mchangamfu pale unapokua umeshiba? Bila shaka wakati wa njaa hua ni dhiki kubwa sana kwako  na haya ndiyo yaliyojiri; Mwili kukosa nguvu,hali inayopelekea kushindwa kufanya kazi,kushiriki michezo. Akili kuchoka haraka na wakati mwingine kushindwa kufanya kazi hali inayopelekea kushindwa kufikiri na kujifunza vizuri. Wengine hupata maumivu ya kichwa. Kinyume cha hayo ni wakati umeshiba unafurahi vizuri hata akili hufanya kazi vizuri hii ni kwasababu mwili umepata nishati kutoka kwenye chakula ulichokula kwa maana nyingine unasema "sasa nina nguvu" . Mwili umendwa na seli ambazo ni mhimili muhimu wa ufanyaji kazi wa mwili.Seli zote za mwili ziwe za misuli,ubongo,ini.. zinahitaji nishati ili ziweze kufanya kazi. Kama seli zitakosa nishati ni wazi kwamba mwili pia hautakua na kazi. Hivyo basi ni muhimu sana...

Mlo kamili(Balanced diet)

 Je tunakula mlo kamili? Jibu lako huenda likawa ndio au hapana na mwingine asijue kabisa kuhusu mlo kamili. Ila maelezo yafuatayo yatatutoa katika kiza na kutuweka kwenye mwangaza juu ya mlo kamili. MLO KAMILI ; ni ule unaozingatia uwepo makundi yote matano ya chakula yaani vyakula vya wanga,protini,matunda,mboga za majani pamoja na vile vya mafuta.                           Na mlo sahihi huenda sambamba na mtindo mzuri wa maisha, kama vile kujiepusha na unywaji wa pombe uvutaji wa sigara matumizi ya dawa za kulevya na mambo mengine ambayo ukiyafanya yanadhuru afya yako.  Na kuzingatia wakati maalum wa kula chakula si kula mara kwa mara inashauriwa hivyo. Kupata mlo sahihi hakuhitaji uwe na pesa nyingi, kwani kuna baadhi wana pesa lakini bado hawafikii mlo sahihi. Ni namna utakavyopangilia ni vipi kwa siku mwili wako utapata faida zinazotokana na makundi yote ya vyakula tuliyotaja hapo juu. Kwa maana tul...