MBOGA /VEGETABLES

Ni matumaini yangu unaendelea vyema na shughuli za kila siku, tukiwa kwenye muendelezo wa faida za vyakula vyetu leo tunaangalia faida zinazopatikana katika mboga za majani.

Iwe asubuhi mchana ama jioni basi hakikisha mlo wako unakuwa na mboga za majani. Imezoeleka sana kwamba kula mboga za majani ni ishara ya kuwa na kipato cha chini hali inayopelekea mboga za majani kubakia kuliwa vijijini na watu wasioweza kununua nyama ama samaki jambo ambalo si kweli, mboga za majani ni kwa watu wote wa rika zote na hii ni kutokana na faida tele zinazopatikana kwenye mboga. Nikushauri tu kama hujawahi kufikiria kula mboga za majni basi fanya kama ilkuwa ndoto na mlo ujao ule mboga za majani.

Ni zipi mboga za majani?

Ni imani yangu tunazifahamu aina nyingi za majani tunazifahamu na ni rahisi sana kupatikana. Si vibaya tukizitaja japo chache; mchicha,sukuma wiki,pilipili boga/hoho,bamia,karoti,giligilani,kabichi,bilingani, nyanya chungu.Tuangalie picha hapo chini bila shaka tuazigundua nyingi.


Kwanini ni muhimu kula mboga za majani?

Kula mboga za majani huupatia mwili faida nyingi za kiafya, watu wenye kupendelea kula mboga za majani huuepukana hatari ya kupata sana na maradhi sugu mfano kukosa choo ama kupata kwa taabu. Vilevile mboga za majani huupatia mwili virutubisho muhimu kwa afya na kuweka hali sawa za kimwili.

Virutubisho

Karibu mboga za majani zote zina kiwango kidogo cha mafuta(fat) na zote hazina mafuta mabaya (cholesterol) hivyo kumfanya mlaji aepuke kupata maradhi yasababishwayo na mafuta kama matatizo ya mzunguko wa damu mafano shinikizo la damu,kuziba kwa mishipa ya damu, unene kupita kiasi.

Mboga za majani zina virutubisho vingi ikiwemo,vitamin A, vitamin C,nyuzinyuzi(fibers),  pamoja madini ya potassium.


  • Madini ya potassium husaidia kudhibiti shinikizo la damu linalotakiwa kiafya.

  • Nyuzinyuzi(dietary fibers) inasaidia kupunguza kiwango cha cholesterol na hupunguza hatari ya mardhi ya moyo. Inasaidia kuondosha ukosefu wa choo au kupata kwa taabu sana. Vilevile hukufanya ujihisi umeshiba ukiwa umekula kiwango kidogo cha nishati hivyo kudhibiti unene kupita kiasi.

  • Folic acid husaidia mwili kutengeneza seli nyekundu za damu ambazo ni muhimu sana kwa usafirishaji wa hewa ya oksijeni ( O2 ) mwilini. Wanawake wanaotarajiwa kupata mimba au wenye mimba wanashauriwa kutumia sana mboga za majni kupata kirutubisho hiki ni muhimu kwa afya yao na afya ya mtoto.

  • Vitamin A vinayafanya macho na ngozi kuwa na afya na kukinga dhidi ya maradhi.

  • Vitamin C husaidia ufyonzwaji wa madini chuma mwilini, husaidia uimara wa fidhi na meno.

Hivyo basi kwa kuepuka madhara kama unene kupita kiasi,kasoro za moyo na mfumo mzima wa mzunguko wa damu,kansa, na kupata mwili wenye afya na nguvu tumia mboga za majani kila unapokaa mezani kutaka kula.

                Nikutakie utekelezaji mwema.


Comments

Popular posts from this blog

VYAKULA VYA WANGA (CARBOHYDRATES)

PROTINI (PROTEIN)