Mlo kamili(Balanced diet)

 Je tunakula mlo kamili?

Jibu lako huenda likawa ndio au hapana na mwingine asijue kabisa kuhusu mlo kamili. Ila maelezo yafuatayo yatatutoa katika kiza na kutuweka kwenye mwangaza juu ya mlo kamili.

MLO KAMILI; ni ule unaozingatia uwepo makundi yote matano ya chakula yaani vyakula vya wanga,protini,matunda,mboga za majani pamoja na vile vya mafuta.                         

Na mlo sahihi huenda sambamba na mtindo mzuri wa maisha, kama vile kujiepusha na unywaji wa pombe uvutaji wa sigara matumizi ya dawa za kulevya na mambo mengine ambayo ukiyafanya yanadhuru afya yako. 
Na kuzingatia wakati maalum wa kula chakula si kula mara kwa mara inashauriwa hivyo.

Kupata mlo sahihi hakuhitaji uwe na pesa nyingi, kwani kuna baadhi wana pesa lakini bado hawafikii mlo sahihi. Ni namna utakavyopangilia ni vipi kwa siku mwili wako utapata faida zinazotokana na makundi yote ya vyakula tuliyotaja hapo juu.

Kwa maana tulio wengi siku inaweza kupita tukiwa tumeishia kula kundi moja tu au mawili kati ya matano, mfano asubuhi ukinywa chai chapati mchana ugali maharage na usiku ukamalizia na wali nyama ni wazi kwamba utakua umepata makundi mawili tu ya chakula yani wanga(chapati,ugali na wali) na protini(maharage na nyama), na kuyaacha makundi mengine ambayo mwili unahitaji.


Kudumu katika hali hii kwa muda mrefu kunapelekea mwili kuwa dhaifu na usio na afya kwakukosa virutubisho muhimu.

Hivyo inashauriwa uwe na kipato cha chini au cha juu jitahidi kuzingatia chakula chako cha kila siku kinahusisha makundi yote ya chakula.

KUZINGATIA MLO SAHIHI KUTAUFANYA MWILI WAKO UWE NA AFYA  IMARA NA KUWEZA KUPAMBANA NA MARADHI.

Tukutane tena wiki ijayo ambapo tutaelezea makundi hayo ya chakula,yanapatikana katika vyakula gani faida zake mwilini. 

Swali lolote tafadhali uliza kwenye comment na usisahau kusubscribe chini hapo ili usipitwe na post yoyote kutoka kwetu.


Comments

Popular posts from this blog

VYAKULA VYA WANGA (CARBOHYDRATES)

MBOGA /VEGETABLES

PROTINI (PROTEIN)