VYAKULA VYA WANGA (CARBOHYDRATES)
Vyakula vya Wanga (Carbohydrates)
(a) Unakua dhaifu na legelege pale unapokua na njaa?
(b) Kwanini unakua hodari na mchangamfu pale unapokua umeshiba?
Bila shaka wakati wa njaa hua ni dhiki kubwa sana kwako
na haya ndiyo yaliyojiri;
- Mwili kukosa nguvu,hali inayopelekea kushindwa kufanya kazi,kushiriki michezo.
- Akili kuchoka haraka na wakati mwingine kushindwa kufanya kazi hali inayopelekea kushindwa kufikiri na kujifunza vizuri.
- Wengine hupata maumivu ya kichwa.
Kinyume cha hayo ni wakati umeshiba unafurahi vizuri hata akili hufanya kazi vizuri hii ni kwasababu mwili umepata nishati kutoka kwenye chakula ulichokula kwa maana nyingine unasema "sasa nina nguvu".
Kama seli zitakosa nishati ni wazi kwamba mwili pia hautakua na kazi.
Hivyo basi ni muhimu sana kujua vyakula gani vitakupatia nishati ya kutosha kwenye mwili ili kuweza kufanya kazi zote zinazohitaji akili na zile zinazotumia nguvu.
Vyakula pekee ambavyo vitaupatia mwili wako nishati ya kutosha ni hivi vya aina ya wanga au (Carbohydrates) kwa lugha ya kitaalamu.
Vyakula vya wanga huchangia karibu asilimia 60% ya nishati yote inayohitajika mwilini.
Kwabahati nzuri sana vyakula hivi vinapatikana kwa wingi sana kwenye maisha yetu ya kila siku mfano wa vyakula hivyo ni mahindi,mihogo,mchele,ngano,ulezi,mtama viazi vitamu,viazi vikuu na vyengine vyenye asili ya hivyo.
Tukutane wiki ijayo ambapo tutajifunza zaidi kiwango gani unatakiwa kuzingatia katika kula yako ya kila siku.
Ahsante nikutakie ufuatiliaji mwema, na usisahau kusubscribe.
Vile vile comment ni muhimu kwa utoaji bora wa makala hizi.
Vile vile comment ni muhimu kwa utoaji bora wa makala hizi.

Good.
ReplyDeleteGood
Delete