JINSI YA KUZUIA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA WAKATI WA UJAUZITO


Utangulizi
Sote ni mashahidi wa kichefuchefu na kutapika hususa wakati wa mimba, kama si mkeo basi huenda akawa dada,shangazi binamu au basi.

Naomba niwatoe wasiwasi na taharuki juu ya hili kwani asilimia kubwa ya wajawazito hupitia hiki kipindi kutokana na mabadiliko makubwa yayofanyika mwilini na zaidi yanachangiwa na vichochezi vya homoni.
Hali hii husababisha wengi wao kudhoofu na kushindwa kufanya shughuli zao kwa kukosa kula ama kula kisha kutapika chakula chote kwani mwili hukosa nguvu.

Nini kifanyike?
Wakati huu usikimbilie famasi kutafuta dawa kwani nako pia hawashauri sana mjamzito kutumia dawa za kuzuia kutapika. Badala yake fanya yafuatayo;

TANGAWIZI
Tangawizi ina uwezo mkubwa wa kuzuia kichefuchefu na kutapika na kuongeza ufanisi wa tumbo kufanya kazi yake ipasavyo.
Jinsi ya kutumia
1.Osha wastani wa vidole vitano vya Tangawizi mbichi ikisha visage vizuri.
2.Chemsha kwenye maji ya ujazo wa lita moja kwa muda usiopungua dakika kumi (10), ikisha chuja vizuri na uhifadhi kwenye themosi(chupa ya chai)
3.Kunywa kikombe kidogo cha chai kutwa mara tatu.(Kamulia ndimu kipande kimoja kwa kila kikombe utakachokunywa.)

Vilevile kata tangawizi kipande chembamba(slice) ikisha kiweke mdomoni kila unapaojihisi kichefuchefu.

 Fanya hivyo hadi utakapoona kichefuchefu na kutapika kumeacha.

Comments

Popular posts from this blog

PROTINI (PROTEIN)

VYAKULA VYA WANGA (CARBOHYDRATES)

MBOGA /VEGETABLES